Domayo aenda kutibiwa Afrika Kusini

Monday December 2 2019

Mwanaspoti-Domayo-Azam-aenda-kutibiwa-Afrika-Kusini-Simba- Yanga

 

By THOMAS NG'ITU

Dar es Salaam. Kiungo wa Azam FC, Frank Domayo wa ameondoka nchini alfajiri ya leo kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwaajili ya matibabu ya tatizo la nyama za paja ya mguu wa kulia.

Domayo alipata majeraha hayo wakati akiwa kambi ya timu ya Taifa iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa Afrika (AFCON) 2021 nchini Cameroon dhidi ya Guinea Ikweta.

Nyota huyo ameambatana na Dokta wa Azam Fc,  Mwanandi Mwankemwa kwa ajili ya matibabu yake yatachukua takribani siku 10.

Matibabua ya Domayo yatafanyika katika hospitali ya Vincent Palotti chini ya Dr Robert Nickolas.

Advertisement