Dk Msolla aunda kamati ya ubingwa Yanga

Muktasari:

Wiki iliyopita Yanga ilitoa taarifa ya kuvunja kamati zote za klabu hiyo na kuwashtua wadau wengi baada ya muda kikosi hicho kikajikuta kikipoteza mechi mbili za ligi.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Yanga, Dk Mshindo Msolla ameunda kamati ya mashindano wenye wajumbe 22 chini ya mwenyekiti Rodgers Gumbo na makamu wake Hamad Islam kwa lengo la kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wiki iliyopita Yanga ilitoa taarifa ya kuvunja kamati zote za klabu hiyo na kuwashtua wadau wengi baada ya muda kikosi hicho kikajikuta kikipoteza mechi mbili za ligi.

Taarifa iliyotoka jioni hii na Katibu Mkuu wa Yanga, Dk David Ruhago imesema kamati ya utendaji ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wao Dk Mshindo Msolla imeunda upya kamati hiyo upya ambayo itaendelea kuongozwa na mwenyekiti Rodgers Gumbo huku Hamad Islam akiendelea kuwa makamu.

Uteuzi huo pia umempa nafasi Deo Mutta kuwa katibu wa kamati hiyo wakati wajumbe wakiwa Mhandisi Hersi Said, Thobias Lingalangala, Said Ntimizi, Mussa Katabalo, Yanga Makaga na Beda Tindwa.

Wengine ni pamoja na Edward Urio, Max Komba, Salum Mkemi, Yusuphed Mhandeni, Adonis Bitegeko, Heriel Mhulo, Mhandisi Issack Usaka, Hassan Hussein, Pelegrinius Rutayuga, Lameck Nyambaya,Kawinda Konde, Eugen Maro na Majid Seleman.