Tshishimbi ajisalimisha Yanga agoma kuzungumza

Thursday March 26 2020

Mwanaspoti, Tanzania, Tshishimbi ajisalimisha Yanga, GSM, Simba SC, agoma kuzungumza

 

By Clezencia Tryphone

Dar es Salaam.Nahodha wa Yanga, Papy Kabamba 'Tshishimbi' leo amejisalimisha ndani ya klabu hiyo kuitikia wito wa viongozi wake.

Tshishimbi aliwasili makao makuu ya klabu ya Yanga saa 6:24 mchana na kukutana na katibu mkuu David Ruhago na kufanya mazungumzo takribani dakika 30.

Tshishimbi aliwasili klabuni hapo na gari yake aina ya Vits akiendeshwa na dereva wake.

Kabla ya kukutana na katibu alianza kuzungumza na Mkuu wa Idara ya Masoko ambapo Tshishimbi alionekana kuongea kwa hasira na baadae kuingia kwa katibu.

Saa 13:23 Tshishimbi alimaliza mazungumzo na katibu na kuondoka zake huku mashabiki waliokuwa nje ya klabu na kuanza kumshangaa.

Nyota huyo aligoma kabisa kuongea na wanahabari na kuingia ndani ya gari lake na kuondoka.

Advertisement

Advertisement