Samatta anaujumbe wako kuhusu corona

Muktasari:

Baada ya virusi vya Corona kusambaa kwa kasi duniani, wachezaji wa mpira wengi wamejifungia ndani na kupost video wakichezea bunda la tishu (toilet paper) kama mpira kwa kupiga danadana na kuonyesha kwamba wamemisi mpira.

MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta anayeichezea klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu nchini England, ameanzisha chalenji yake binafsi ya pakti ya majani ya chai (Tea Bag Challenge) baada ya kujifungia ndani akikwepa virusi vya ugonjwa wa Corona.
Iko hivi baada ya virusi vya Corona kusambaa kwa kasi duniani, wachezaji wa mpira wengi wamejifungia ndani na kupost video wakichezea bunda la tishu (toilet paper) kama mpira kwa kupiga danadana na kuonyesha kwamba wamemisi mpira.
Lakini kwa upande wa Samatta yeye ametoa kali ya mwezi baada ya kuposti video ambayo yupo jikoni akitengeneza chai, anatoa kipakti kimoja cha majani ya chai na kukiangushia mguuni na kukipiga teke moja na kinaingia moja kwa moja kwenye kikombe cha chai kilichopo juu ya meza na kisha anatia maji kikombeni humo na kukoroga chai na kuinywa
Baada ya Samatta kuweka video hiyo, wachezaji wenzake walionekana kumuunga mkono, ambapo Saimon Msuva na Nickson Kibabage wanaocheza soka la kulipwa nchini Morocco katika klabu ya Diffaa Al Jadida wao pia waliweka video zao wakifanya kama Samatta.
Kiungo Abdallah Khamis anayeichezea klabu ya Orapa Utd inayoshiriki Ligi Kuu nchini Botswana naye aliweka video yake akifanya jambo hilo kama Samatta
Wakati hawa wakiunga mkono chalenji hiyo, wachezaji wengine wao wameendelea na chalenji ya kutumia karatasi laini za chooni (toilet paper) kupiga danadana akiwamo Ibrahim Ajibu alionyesha ufundi zaidi hadi kuirusha na kuipoza nyuma ya shingo.Shaban Chilunda wa Azam Fc naye ametisha kwa danadana.