Msuva anahesabu saa tu huko

NI suala la muda tu inaelezwa kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva kuondoka Morocco na kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa klabu ya Ligi Daraja Kwanza nchini Ufaransa, Le Havre ni imetuma ofa ya kumsajili nyota huyo wa zamani wa Yanga ya Ligi Kuu Bara.

Hivyo inaelezwa kuwa Msuva yupo mbioni kuondoka Morocco kumeanza tena kuzua majadala kuwa huenda mshambuliaji huyo akatimkia zake Ufaransa kutokana na Ligi Kuu Morocco kumalizika huku Raja Casablanca wakitwaa ubingwa.

Katika hilo, Msuva aligomea ni wapi ambako anaweza kwenda lakini alisema lolote linaweza kutokea,

“Itakuwa kama sapraizi kwa Watanzania ningependa wasubiri na kuona nini kitatokea,” alisema.

Msuva akiwa na chama lake la Difaa waliwahi msimu mmoja kwenda kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya huko Hispania lakini alitokea kuzivutia klabu kadhaa ambazo walicheza nao michezo ya kirafiki lakini sasa mambo yanaonekana