Msiba wa MV Nyerere waigusa Malaika Band

Muktasari:

  • Meneja wa bendi hiyo King Dodoo amesema,wamesimamisha onyesho hilo kutokana na msiba uliotokea mkoani Mwanza baada ya kivuko cha MV Nyerere kupinduka na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

Bendi ya muziki ya Malaika chini ya kiongozi Christian Bella imeahirisha onyesho la Family Bonanza, linalofanyika kila siku ya Jumapili katika Ukumbi wa Msasani Beach Kawe, Dar es Salaam.

Meneja wa bendi hiyo King Dodoo amesema,wamesimamisha onyesho hilo kutokana na msiba uliotokea mkoani Mwanza baada ya kivuko cha MV Nyerere kupinduka na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

King Dodoo amesema haitakuwa busara kwa msiba mkubwa kama huo, kufanya onyesho wakati Watanzania wakiwa na majonzi, hivyo wameamua kusitisha onyesho hilo ili kuungana nao.

“Tumeamua kusimamisha onyesho kutokana na ajali ya Mv Nyerere iliyotokea huko Mwanza, tumeona ni jambo jema kuungana na wenzetu waliofiwa kuomboleza msiba huu. Tumeona sio jambo jema tuendeleze burudani, ”amesema King Dodoo.