Mshindi wa SportPesa akabidhiwa ndinga lake

Wednesday November 6 2019

Mshindi - SportPesa -Tarimba-Abbas-mkurugenzi-akabidhiwa -ndinga -Yusuph -Jacksoni -Murimi -

 

By Mwandishi wetu

MKAZI wa Serengeti kijiji cha Mugumu, Yusuph Jacksoni Murimi (29) amekabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid mara baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya Faidika na Jero.

Promosheni hiyo ilidumu kwa siku 40 na watumiaji wa mtandao wa Tigo kupitia huduma ya TigoPesa walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo simu janja za mkononi (smartphone) kila siku na promosheni ya mwisho ilikuwa ni zawadi ya gari.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Yusuph alisema “Ukirudia mazungumzo yangu siku ya kwanza wakati napigiwa simu utagundua nilikuwa siwaamini walionipigia simu kama ni kweli SportPesa maana siku hizi mjini watu hawatabiriki. Nilikuwa nacheza tu lakini sikutarajia bahati hii ya ushindi wa gari itanidondokea.

“SportPesa wamenipa mapokezi mazuri ikiwemo kusimamia gharama zote kuanzia usafiri wa ndege, malazi pamoja na matumizi ya siku nzima na kuhakikisha gari langu linapata usajili kupitia jina langu na kukabidhiwa.”

“Sijui nisemeje lakini nawashukuru SportPesa, mimi ni mwajiriwa kwenye kampuni kama fundi welder na sikutarajia kama siku ningeshinda zawadi ya gari.”

“Nawasihi vijana wenzangu wacheze na SportPesa maana kwa sasa nawaona hawana mpinzani, sio kama unapoteza pesa. Mimi nilikuwa nacheza na kushinda kwa kubashiri mechi kama sehemu ya burudani lakini leo nimejionea dhahiri kuwa kuna zaidi ya ushindi,” alisema.

Advertisement

Kwa upande wa SportPesa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania,Tarimba Abbas alisema: “SportPesa inazidi kuwafungulia dunia wateja wake hasa kupitia promosheni mbalimbali kwa simu ya mkononi unaweza kufanya maajabu yanayoweza kubadili maisha yako.”

“Napenda kumpongeza sana Yusuph kwa ushindi wake na kujinyakulia gari mpya aina ya Renault Kwid na kuweza kuitumia kujiingizia kipato na shughuli nyingine za kujenga taifa.”

“Hivyo basi Watanzania wakae mkao wa kula mambo mazuri zaidi yanakuja kutoka SportPesa ili kuwaongezea burudani wateja wetu,” alisema Tarimba.

Mwakilishi kutoka Tigo, Ikunda Ngowi naye alisema

“Nampongeza mshindi wetu nawaasa Watanzania waendelee kucheza na SportPesa kupitia mtandao wa tigo maana mambo mazuri ni mengi.”

Advertisement