Mshikamano yajipa matumaini kutinga Ligi Kuu

Sunday November 12 2017

 

By Charles Abel

PAMOJA na kuachwa kwa tofauti kubwa ya pointi na timu mbili zilizo juu ya msimamo wa kundi A, Mshikamano FC bado ina matumaini ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Timu hiyo ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa kundi A ikiwa na pointi tisa huku vinara wakiwa ni JKT Ruvu ambao kabla ya mechi yao jana dhidi ya Ashanti United walikuwa na pointi 22 na African Lyon wako nafasi ya pili na pointi 17.

Kocha wa Mshikamano FC, Chiki Mchome alisema michezo miwili inayofuata ndio itatoa taswira ya nafasi yao kwenye msimu huu kama watapanda au hawatopanda Ligi Kuu.

"Bado hatujakata tamaa kwa sababu mechi tano zilizobakia ni nyingi na wapinzani wetu wanaweza kupoteza kama ambavyo African Lyon walivyopoteza na sisi.

Kocha huyo alisema ataimarisha timu yake katika dirisha dogo la usajili kwa kusajili wachezaji watano akiamini watakuwa na msaada kwa kikosi chake kwenye mechi tano zilizo