Mputu: Tunajua Simba ni timu bora zaidi nyumbani

Muktasari:

Alipotoka ndani ya Uwanja wa ndege Mputu alikuwa mchezaji pekee ambaye alishangiliwa na kulindwa na mashabiki zaidi ya wachezaji wote.

Dar es Salaam.  Mshambuliaji Tresor Mputu amekuwa kivutio wakati kikosi cha TP Mazembe kimewasili jijini Dar es Salaam ukiwa ni msafara wa wachezaji 18 na viongozi 13.

Mara baada ya kuwasili msafara huo wachezaji walitoka ndani mmoja mmoja huku mashabiki wao wakizuiwa kuwagusa wachezaji hao.

Mashabiki hao walikiwa wakizuia kila mchezaji anayetoka ndani hawakutaka aguswe wala kuongea na mtu yoyote.

Alipotoka ndani ya Uwanja wa ndege Mputu alikuwa mchezaji pekee ambaye alishangiliwa na kulindwa na mashabiki zaidi ya wachezaji wote.

Mputu mara baada ya kuwasili alisema wanafahamu wanakuja Tanzania kucheza na timu nzuri ambayo imeonesha ushindani katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mputu alisema Simba ni timu nzuri haswa inapocheza katika uwanja wake wa nyumbani wamejipanga kushindana nao kwani hautakuwa mchezo mwepesi kwa pande zote mbili.

Alisema Simba wamewafunga AS Vita ambao nao wanatoka DR Congo wanalifahamu na wamejipanga vizuri kulikabili hilo.

"Tumekuna kushindana hapa ugenini ili kupata matokeo ambayo yatakuwa na faida kwetu kwenda kuturahisishia katika mchezo wa marudiano nyumbani," alisema Mabi.