Mpepo kuikosa FA

Friday June 14 2019

 

By Eliya Solomon

STRAIKA wa kimataifa wa Tanzania, Eliuter Mpepo anayeichezea  Buildcon ya Zambia, ataukosa mchezo wa kesho Jumamois wa robo fainali ya Kombe la FA nchini humo dhidi ya Zesco United iliyo chini ya kocha George Lwandamina.
Mpepo ambaye  huu ni msimu wake wa kwanza akiwa na   Buildcon, aliseme ameshindwa kusafiri na timu kwani anasumbuliwa na  ugonjwa wa Malaria.
“Nilitamani kuwa sehemu ya mchezo lakini sina namna kikubwa ni kujiuguza na kuiombea dua timu yangu ishindi mchezo huo.
“Ushindi utatufanya kuingia nusu fainali, wote tunacheza ugenini uwanja wa Mashujaa, Lusaka,” alisema mshambuliajio huyo.
Akiuzungumzia msimu wake wa kwanza nchini humo, Mpepo alisema amejifunza vitu vingi ambavyo anaamini vimemuimarisha na kuwa mchezaji mwingine.
“Bado nina safari ndefu kwenye soka, kila siku nimekuwa nikijifunza vitu vipya,” alisema.

Advertisement