Mourinho, Kane kulimwa mishahara

Muktasari:

Mourinho anapokea mshahara wa Pauni 290,000 kwa wiki kwenye klabu hiyo, wakati Kane analipwa Pauni 200,000 kwa wiki.

LONDONENGLAND . JOSE Mourinho na mastaa wake huko Tottenham Hotspur watalazimika kukatwaa mishahara yao baada ya bosi Daniel Levy kusema kwamba itabidi wapunguza machungu ya gharama za kuendeesha timu kutokana na janga la virusi vya corona.

Spurs itakuwa timu ya pili kwenye Ligi Kuu England baada ya Newcastle kukataa mishahara ya wachezaji wao wasiocheza.

Zaidi ya watu 550 wameshuhudia mishahara yao imekatwa kwa miezi miwili sasa.

Mwenyekiti wa Spurs, Levy amewaambia Mourinho, Harry Kane na wachezaji wengine kwenye kikosi hicho kwamba itakapolazimika kukata mishahara basi atafanya hivyo.

Mourinho anapokea mshahara wa Pauni 290,000 kwa wiki kwenye klabu hiyo, wakati Kane analipwa Pauni 200,000 kwa wiki.

Levy, ambaye msimu uliopita alikuwa mmoja wa mabosi wanaolipwa pesa nyingi kwenye Ligi Kuu England, Pauni 7 milioni, alisema: “Uendeeshaji wa klabu umesimama, watu wetu wengine wamepoteza kazi, hivyo hali ni mbaya. Gharama za klabu kwa mwaka ni mamilioni ya pauni.

“Tumeona baadhi ya klabu kuba duniani kama Barcelona, Bayern Munich na Juventus zimechukua hatua ya kupunguza gharama.”

Wakati huo huo, Spurs imepigwa faini ya Pauni 18,000 baada ya Uefa kumlaumu kocha Mourinho kuwa alichelewesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya RB Leipzig kwa dakika tatu.

Wasiwasi mwingine unaowakabili Harry Kane amewaambia ataondoka kama hakutakuwa na mabadiliko kwenye timu.

Kuna wasiwasi pia beki Jan Vertonghen anaweza kuachana na timu hiyo bure mwishoni mwa msimu huu baada ya kugomea mkataba mpya huku Ajax wakitaka kumsajili.