Morrison atuliza mzuka Simba

Wednesday August 12 2020

 

By THOBIAS SEBASTIAN

SAKATA la mshambuliaji wa mpya wa Simba, Bernard Morrison bado linaendelea dhidi ya waajili wake wa zamani Yanga.

Watanzania wengi haswa wale ambao wapenda soka wanasubiri kwa hamu hatma ya sakata la Morrison ambalo litatolewa na kamati ya sheria na hadhi za wachezaji, iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Elias Mwanjala.

Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa (Twitter), Morrison aliweka video akiwa anapiga mpira danadana huku akiandika maneno mafupi.

Maneno hayo ambayo alaindika Morrison, akiambatanisha na video hiyo ni (Kuweni wapole, msiwe na presha) huku kukiwa na picha ndogo iliyokuwa inaonyesha sura ya mnyama Simba.

Maneno hayo huenda yakatuliza presha na mzuka kwa mashabiki wa Simba ambao wanatamani kumuona anashinda shauri lake dhidi ya waajiri wake wa zamani Yanga kwani ujumbe huo umeambatana na picha pamoja kauli mbio ya timu hiyo inayosema Simba nguvu moja.

Muda wowote kwa mujibu ya Mwanjala, hukumu ya sakata hilo la Morrison linaweza kutolewa na kumfahamu aliyeshinda kati yake na Yanga, ambao wameeleza wazi kuwa mchezaji huyo alisaini mkataba wao mpya wa miaka miwili baada ya ule wa awali wa miezi sita kuwa unaelekea ukingoni.

Advertisement

Advertisement