Morrison apelekwa Kamati ya Nidhamu

Muktasari:

Kwa upande wa Azam FC  wametozwa faini ya Sh 1 milioni kwa kosa kuchelewa kutoka uwanjani hata Kamishna alipowaita walikaidi amri ya kutoka vyumbani na golikipa wa timu hiyo kuchelewa zaidi na alipofika uwanjani kushindwa kuwapa mikono timu pinzani (Coastal Union) kwenye mchezo uliofanyika February 15 mwaka huu uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Azam wamepewa adhabu hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 14(43) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

MSHAMBULIAJI  wa Yanga, Bernard Morrison amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons, Jeremia Juma wakati mpira ukiwa umesimama.
Morrison afanya tukio hiyo Februari 15 mwaka, mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo timu hizo zilitoka sare tasa.

Wakati Morrison akipelekwa Kamati ya Nidhamu, timu yake imetozwa faini ya Sh 500,000 kwa kosa la kushindwa kuwasilisha fomu ya wachezaji wao kwenye kikao cha awali cha mchezo huo 'Pre match meeting'. Adhabu waliyopewa Yanga ni kwa kuzingatia kanuni ya 14 (3) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Kwa upande wa Azam FC  wametozwa faini ya Sh 1 milioni kwa kosa kuchelewa kutoka uwanjani hata Kamishna alipowaita walikaidi amri ya kutoka vyumbani na golikipa wa timu hiyo kuchelewa zaidi na alipofika uwanjani kushindwa kuwapa mikono timu pinzani (Coastal Union) kwenye mchezo uliofanyika February 15 mwaka huu uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Azam wamepewa adhabu hiyo kwa mujibu wa Kanuni ya 14(43) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Uamuzi huo ulitolewa kwa timu ya Yanga, Azam na Morrison ni kwa mujibu wa Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi  iliyokutana jana Ijumaa na kupitia taarifa mbalimbali za mechi ya Ligi Kuu Vodacom (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) zinazoendelea hivi sasa.

Baada ya kupitia mechi hizo kamati hiyo imeshusha rungu kwa baadhi ya klabu za ligi kuu baada ya kukutwa na makosa mbalimbali.