Mo Rashid hajutii kuwepo Simba

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mohammed Rashid

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa Simba, Mohammed Rashid 'Mo Rashid' amesema, hana wasiwasi ndani ya kikosi cha Simba kwa sababu utafika wakati wake wa kucheza, anachojua anazokutana nazo ni changamoto tu.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mohammed Rashid 'Mo Rashid' amesema hajutii kuwepo ndani ya timu hiyo licha ya kutopata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.
Mo Rashid alisajiliwa Simba akitokea Tanzania Prisons ambako alikuwa kikosi cha kwanza katika mechi zote na alicheza kwa dakika zote 90, jambo lililomfanya aitwe kwenye kikosi cha Taifa Stars.
Lakini, tangu ajiunge na Simba msimu huu, hajapata nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza ambapo Mo anafafanua.
"Nimekuja Simba mwenyewe sikulazimishwa na mtu mwingine yeyote kwa nini nijute. Kikubwa ni kujipanga na kuchukulia hii ni sehemu ya changamoto katika maisha yangu,"alisema Mo Rashid.
Amesema, anajua sababu ni kuingia Simba na kukuta tayari kuna washambuliaji ambao wanaamiwa na wenye uzoefu kwenye soka kwa kipindi kirefu.
"Kila kitu ni kukipa muda kwani utafika wakati wangu wa kuaminiwa kwenye timu nitacheza, hilo sina wasiwasi nalo kwa sababu najua