Mnguto alia uhaba wa mashabiki viwanjani

Muktasari:

Ametaja vitu vinne ambavyo ni  kubadilika kwa ratiba mara kwa mara, usumbufu wa viwanja, matumizi ya tiketi za halmashauri na kukosekana kwa watazamaji Uwanjani.

Kati ya vitu muhimu alivyozungumzia  mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Steven Mnguto ni watazamaji kukosekana Uwanjani.
Katika hutuba ya Mnguto kuna vipengele alivyoeleza kwamba kwamba kuna vikwazo vinavyotokea kwenye soka na akiahidi wanapanbana navyo.
Ametaja vitu vinne ambavyo ni  kubadilika kwa ratiba mara kwa mara, usumbufu wa viwanja, matumizi ya tiketi za halmashauri na kukosekana kwa watazamaji Uwanjani.
"Tulidhani tiketi za halmashauri zingekuwa mkombozi katika suala zima la mapato lakini imekuwa kinyume chake," amesema Mnguto na kuongeza;
"Matokeo yake ni malalamiko ya wizi na kuchelewesha malipo, lakini viwanja vingine vinavyotuumiza Sana ni viwanja vyetu vikubwa viwili vinavyohudumiwa na serikali."
"Uwepo wa Selcom haututendei haki kabisa kuna kadhia nyingi zinazotokea na tunajaribu kutafuta namna bora ya kupata tiketi ambazo zitatusaidia," amesema.
Pia amewaomba radhi kutokana na usumbufu wa viwanja ambavyo amesema havina ubora unaotakiwa "Jitihada ya kuboresha halipo na wala hatupati ushirikiano na wahusika,"amesema.