Mkwasa agundua mawili Yanga

Muktasari:

Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi kwa mara ya kwanza leo jioni huku kocha Boniface Mkwasa akisimamia.

Kikosi cha Yanga kimefanya mazoezi ya kwanza leo, jioni katika uwanja wa shule ya sheria jijini jirani na kituo cha daladala cha Ubungo Mawasiliano (Simu 2000).

 

Kocha msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema amegundua mambo mawili katika mazoezi ya kwanza ambayo wamefanya leo.

 

Mkwasa amesema jambo la kwanza ambao ameliona kwa wachezaji wake kuwa walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu zaidi.

 

Anasema wachezaji wengi kati ya hawa walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu kuliko kucheza mpira.

 

"Kwa maana hiyo ni shida ya kwanza ambayo imeonekana kwetu katika mazoezi ya leo ambayo tutakwenda kulifanyia kazi," anasema.

 

"Tatizo hilo limetokana na wachezaji kuonekana kufanya mazoezi ya nguvu kama 'beach' na maeneo mengine.

 

"Jambo la pili ambalo nimeliona wachezaji wangu wengi wamepoteza uwezo wa kumiliki mpira kwani mchezaji akiwa na mpira mguuni inakuwa ngumu kuwa salama kwa asilimia kubwa na badala yake hupoteza.

 

"Wakati huo huo nimeona wachezaji wakipoteza pasi mara kwa mara na limetokana kupoteza uwezo wa umiliki mpira.

 

" Kama benchi la ufundi tumeliona hilo na tunazidi kulifanyia kazi ili kila kitu kwenda sawa," anasema Mkwasa.