Mkwasa achukuwa nafasi ya Mayanga

Friday August 14 2020

 

By Thobias Sebastian na Olipa Assa

KLABU ya Ruvu Shooting imeachana na kocha wao Salum Mayanga na kumpa ajira kocha Boniface Mkwasa.
Mkwasa msimu uliopita alikuwa akikinoa kikosi cha Yanga akiwa kocha wa muda na baadae akawa msaidizi wa Luc Eymael ambae naye alitimuliwa.
Afusa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ameithibitishia Mwanaspoti Online leo Ijumaa Agosti 14, 2020 kuwa Mkwasa ni kocha mkuu mpya wa kikosi hicho.
Masau amesema wamemalizana vizuri na Mayanga ambaye mkataba wake ulimalizika na ameshukuru kwa utendaji kazi wake mzuri.
"Maamuzi yetu kama uongozi tumekubaliana na Mkwasa kuja kuifundisha timu yetu, kwa mkataba ambao hautaelezwa muda wake kwani ni makubaliano ya pande mbili," amesema.
"Baada ya kumpata Mkwasa kama kocha wetu mkuu ndio tutaanza masuala ya usajili kwa kuangalia mapendekezo yake kwani yeye ndio atakuwa na timu,"
"Tunaimani chini ya Mkwasa kwa uzoefu wa soka la Tanzania aliokuwa nao tangu akiwa anacheza mpaka kufundisha tutafanya vizuri msimu ujao," amesema Masau
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Mkwasa kuifundisha Ruvu Shooting kwani aliwahi kuifundisha miaka ya nyuma na kuachana nayo alipokwenda kuwa msaidizi wa Hans Pluijm alipokuwa Yanga.
xxxx

Advertisement