Mkude, Kagere wapewa mazoezi maalumu

Muktasari:

Kikosi cha Simba, kinaendelea na maandalizi hayo Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inaendelea Kisiwani humo pamoja na michuano mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Unguja. Kiungo wa Simba, Jonas Mkude jana Jumapili alijiunga na timu yake iliyopo Kisiwani Zanzibar ikishiriki mashindano ya Kombe la Mapinduzi akitokea jijini Dar es Salaam alikokuwa na matatizo ya kifamilia.
Mkude amechelewa kujiunga na kikosi hicho kwa sababu ya matatizo hayo ambapo ilielezwa kuwa alifiwa na kaka yake.
Baada ya kujiunga na wenzake leo Jumatatu asubuhi alifanya mazoezi yake ya kwanza ambapo aliambiwa akimbie kuzunguka uwanja.
Wakati Mkude akipewa mazoezi hayo maalumu kabla ya kuanza kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake straika Meddie Kagere naye alifanya mazoezi maalumu ili kujiweka fiti kwa kukimbia kuzunguka uwanja.
Kagere alifanya mazoezi hayo pamoja na yale ya kuchezea mipira chini ya kocha wa viungo Zrane Adel.