Mkongo Simba uhakika

Tuesday July 10 2018

 

By MWANAHIBA RICHARD

SIMBA imeshusha kiungo Kakule Mugheni Fabrice kutoka Rayon Sports ya Rwanda na kocha wa timu hiyo Masoud Djuma amesema kiungo wake si wa majaribio bali anasaini mkataba wa kuitumikia Simba kwani kiwango chake ni kizuri.
Djuma aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yao yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veteran kwamba anamfahamu Fabrice kwani ameishi naye miaka miwili hivyo ameleta kiungo mwenye uwezo ambapo Fabrice naye alianza mazoezi ya pamoja kwa mara ya kwanza.
Djuma alisema ujio wa kiungo huyo unaweza kuwapa nafasi wachezaji wengine kwenda kujaribu maisha kwenye klabu nyingine kuliko kukaa ndani ya Simba bila kupata namba. Haruna Niyonzima ni miongoni mwa nyota wanaotajwa kutemwa kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya muda mrefu.
"Kuna wachezaji wataachwa ama wengine kupelekwa kwa mkopo timu zingine kutokana kuwa wana mikataba na Simba,  huwezi kuwa na mchezaji ambaye hapati nafasi ya kucheza halafu unaendelea kukaa naye huko ni kuuwa kipaji chake ni bora umpe nafasi ya kwenda kucheza kwingine.
"Mfano kipa Mseja huyo hawezi kuendelea kuwepo maana tayari kuna makopa wengine ambao wataendelea kumkalisha nje,  hivyo tutamruhusu na ndiyo maana hayupo mazoezi na sio huyo wapo wengi tu muda ukifika watawekwa wazi ika huyu kiungo hajaja kwenye majaribio nimemleta kuja kupiga kazi, kitu ambacho kitafanyika kwa huyu kchezaji ni kumpiga afya yake tu," alisema Djuma

ISHU YA WAWA
Djuma alisema ni lazima kikosi chake kuwa na nyota wengi vijana lakini na watu wazima kwa maana wenye umri mkubwa kama Paschal Wawa wawepo.
"Huwezi kumwangalia mtu kwa mechi moja ama mbili halafu ukasema hafai,  Wawa ni beki mzuri na ikumbukwe hakucheza muda mrefu kadri siku zinavyozidi kwenda mbele anakuwa bora, Wawa sio mzee kwamba hawezi kucheza watu wafahamu hilo,"alisema Djuma

Advertisement