Mirambo amtikisa kocha Muangola

Tuesday April 30 2019

 

By Thomas Ng'itu

NDIO Serengeti Boys ilitolewa mapema katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana U17 2019 zilizofanyika Tanzania na Cameroon kubeba taji kwa kuigonga Guinea kwa mikwaju ya penalti, lakini kocha wa kikosi hiyo Oscar Mirambo ametikisa fainali hizo.

Kocha wa Angola waliomaliza kama washindi wa tatu wa fainali hizo za 13, Pedro Goncalves ameshangazwa na namna ambavyo mashabiki wa Tanzania walivyomgeuka kocha Mirambo baada ya matokeo mabovu wakati ye mwenyewe amemkubali kinoma.

Goncalves alisema mpira ni kitu cha maendeleo na siyo hatua za haraka kama watu wengi wanavyodhani kwani hata yeye alianza kuitengeneza timu kwa muda mrefu na kutaka Watanzania wajue Mirambo ni hazina na kama watampa muda ataibeba nchi baadaye.

“Shirikisho lilinipa muda wa kuwaandaa vijana kwani wanajua vijana wanatokea huku chini, leo tupo tumeingia Kombe la Dunia na tumefanya vizuri Afcon hiki ni kitu tulichojiandaa kwa muda mrefu,” alisema.

Advertisement