Migne amrudisha winga AF Leopards

Muktasari:

Ingwe walilazimika kutoka goli moja nyuma baada ya kuwahiwa mapema na bao lake Ken Nambute katika dakika za mwanzo mchezoni.

WINGA machachari Paul Were aliyerejea kwenye Ligi ya KPL na kujiunga na klabu yake ya zamani AFC Leopards, kafichua kuwa kocha wa Harambee Stars Sebastian Migne ndiye aliyemvuta kutoka majuu alikokuwa akipiga soka lake la kulipwa.

Juzi Alhamisi Were alianza shughuli vyema kwa kuisaidia Inge kuwalima Posta Rangers magoli 3-1.

Kwenye mechi hiyo, winga huyo anayesifika kwa kasi yake, alionyesha bado yupo kwenye ubora wake baada ya kutoa asisti ya bao la tatu lililofungwa na kiungo mshambuliaji Whyvonne Isuza.

Ingwe walilazimika kutoka goli moja nyuma baada ya kuwahiwa mapema na bao lake Ken Nambute katika dakika za mwanzo mchezoni.

AFC walisawazisha kupitia Brian Marita baada ya kipa wa rangers kushindwa kuidhibiti mkiki wake mzito.

Dadika tano kabla ya kwenda mapumzikoni nahodha wa Ingwe Robinson Kamura alitia la pili baada ya blanda ya kipa Lule.

Presha zaidi kutoka kwa Were aliyekuwa akicheza mechi yake ya pili tangu kurejea, kiungo straika Isaac kipyegon na Isuza ambao mara kwa mara walibadilisha pasi za kupendeza mchezoni, zilishia kuwapa bao la tatu.

Baada ya ushindi huo, Were alibaki kusifia uwezo wake huku akifichua kwamba anajitahidi sana ili kuhakikisha anapata namba kwenye kikosi cha Stars kinachoelekea Cairo, Misri kwa ajili ya dim,ba la AFCON 2019

“Nilifurahia mchango nilioutoa kwa timu kwenye mechi yangu ya pili toka nimerejea. Wajua sababu yangtu mimi kurudi ilichochewa na familia yangu lakini zaidi kocha Sebastian Migine aliyeniambia alitaka kunifuatlia kwa karibu. Ndio sababu niliamua kurejea ka kuwa hata kule majuu pia kunazo chanamoto” Were akasema.

Were alijiunga na Ingwe kwa mkataba wa miezi minne baada ya kuikacha klabu yake ya Uturuki, Trikala inayoshiriki kwenye divisheni ya pili yan soka nchini humo.