Mechi ya Biashara, Alliance mtoto hatumwi dukani leo

Wednesday May 15 2019

 

By Thomas Ng’itu

LEO jioni majira ya saa kumi nyasi za uwanja wa Karume, Musoma zitawaka moto kwa kuikutanisha Biashara Utd dhidi ya Alliance mchezo ambao unatarajia kuwa mkali.

Biashara wanashika nafasi 18 wakiwa na pointi 40 katika michezo 34, huku Alliance wanashika nafasi 15 wakiwa na pointi 41 katika michezo 35 hivyo kila timu inahitaji ushindi katika mcheoz huu ili kusogea juu.

Iwapo Alliance ikakubali kichapo dhidi ya Biashara watashuka mpaka nafasi ya 17 kutokana na kucheza michezo 36, huku Biashara kama wataibuka na ushindi katika mchezo huo watasogea mpaka nafasi ya 14 kwani watakuwa na pointi 43.

Mchezo huo pia ulikuwa ukighailishwa mara kwa mara kwahiyo kucheza kwao leo kutakuwa kunakata hamu ya mashabiki wa Musoma ambao walikuwa wanasubilia kwa hamu mechi hiyo.

Biashara katika mechi zao zote za nyumbani msimu huu, imefungwa na Mwadui pamoja na Simba hivyo Alliance watakuwa na kazi ya ziada katika uwanja huo wa Karume,Musoma.

Mechi zingine zinazopigwa leo, Mbeya City vs Coastal Union na Kagera Sugar dhidi ya Stand United.

Advertisement

Advertisement