Mchezaji afariki dunia uwanjani, Amissi Tambwe athibitisha!

Friday April 26 2019

 

 Summary:Papy Faty amekutwa na umauti akiwa uwanjani wakati aliitumikia klabu yake katika mechi ya ligi. Kiungo raia wa Burundi Papy Faty amefariki jana Alhamisi jioni baada ya kuanguka akiwa uwanjani aliitumikia klabu yake mchezaji mwenzake Amissi Tambwe amethibitisha.

Taarifa kutoka nchini Eswatini zinasema Faty amekutwa na umauti wakati akiitumikia timu yake ya Melanti Chiefs ilipokuwa ikicheza nyumbani dhidi ya Black Mamba.

Awali kiungo huyo alilazimishwa kupumzika kucheza soka kwa muda wakati akiwa klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini mwaka 2016 baada ya kugundulika kuwa na matatizo ya kiafya hasa sehemu ya moyo.

Mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe amethibitisha taarifa hizo za kifo cha Faty baada ya Shirikisho la Soka Burundi kuwajulisha kundi la wachezaji wa taifa hilo.

"Nikweli Faty amefariki dunia,imetusikitisha sana unajua ndiyo alianza kucheza baada ya kuambiwa apumzike kwa muda mrefu, ameelezea Tambwe.

Faty alikuwepo katika kikosi cha Intamba m'Urugamba kilichofuzu Fainali za Mataifa Afrika kilichotoa sare dhidi ya Gabon na kufuzu kwa mara ya kwanza fainali hizo.

Advertisement

Advertisement