Mbelgiji Simba tumeamishia nguvu zetu zote Ligi Kuu

Wednesday August 28 2019

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba imeamisha nguvu katika Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

Kocha wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems alisema kuondolewa kwao katika Ligi ya Mabingwa wameamishia nguvu katika mashindano mengine.

Aussems alisema kesho Alhamisi tunacheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara wataitumia kurudisha morali na hali ya ushindani katika timu.

"Tumetoka kupata matokeo mabaya ambayo hayakuwa matarajio yetu katika mechi na UD Songo ambayo yameshusha morali ya timu na hali ya kushindana kwa wachezaji.

"Kwa maana hiyo ili kurudi katika hali yetu ya ushindani tunataka kutumia mchezo huu ili tushende jambo ambalo litawarudisha katika hali nzuri," alisema.

"Sambamba na hilo tumeamishia nguvu zetu katika Ligi Kuu Bara 'VPL', kombe la shirikisho 'FA' na mashindano mengine ambayo yote tumepanga kufanya vizuri," alisema Aussems.

Advertisement

Advertisement