Mbelgiji Simba awatema Kaheza, Mo Rashid CAF

Muktasari:

Kaheza, Mo Rashid wamesajiliwa na Simba msimu huu lakini tangu wametua katika kikosi hicho wameshindwa kuwa ya namba za kudumu katika kikosi cha kwanza cha Mbelgiji

Dar es Salaam. Kocha wa Simba Patrick Aussems amewatema washambuliaji Mohamed Rashid na Marcel Kaheza katika kikosi chake kitakachoshiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yatakayoanza hivi karibuni.

Simba imepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka mitano iliyopita.

Viongozi wa Simba walikabidhiwa majini ya wachezaji hao na kocha mkuu Mbelgiji Aussems wamethibisha kuwaacha wawili hao kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.

Wachezaji wengine ambao majina yao yamepelekwa CAF ni Aishi Manula, Deogratius Munishi, Mohamed Hussein, shomary kapombe, Erasto Nyoni, Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, John Bocco, Pascal Wawa, James Kotei, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Clatous Chama, Juuko Muurshid, Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Adam Salamba, Haruna Niyonzima.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' alikiri kupeleka kikosi chao TFF na kwamba hivi karibuni watatangaza wachezaji watakaiwakilisha Simba na wale watakaobaki ikiwa ni pamoja na sababu za kuwaacha.

"Tulipeleka majina muda mrefu bado kuyatangaza tu, ila tutayatangaza hivi karibuni," alisema Try Again ambaye hakuwa tayari kuweka wazi walioachwa na wale watakaoingia kwenye vita hiyo ya kimataifa.