Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashemeji Derby: Gor Mahia na AFC Leopards situation kwa ground itakuwa different

Muktasari:

Mechi ya Jumapili itakuwa ya 86 kukutanisha miamba hawa, na ya kwanza kwa msimu huu. Gor Mahia kwa sasa iko katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 15, baada ya kushuka dimbani mara tano, pointi moja nyuma ya vinara Tusker FC wenye 16 baada ya mechi nane.

Nairobi, Kenya. Wikiendi hii, wakati kukiwa na shughuli kubwa pale Stamford Bridge England kati ya wenyeji Chelsea ya Frank Lampard na Crystal Palace ya Roy Hogson, Jijini Nairobi kutakuwa na vita!

Sio vita ya mapanga na mishale. Sio vita vya dunia. Sio vita vya mangumi na mateke, vitakuwa ni vita vya miamba wawili wa soka la Kenya, Gor Mahia na AFC Leopards.

Kuanzia saa tisa alasiri, Novemba 10, Dimba la Moi Kasarani litashuhudia mechi bab’kubwa katika historia ya soka la Kenya. Historia ya Mashemeji hawa haijaanza leo. Tangu walipokutana kwa mara ya kwanza Mei 5, mwaka 1968 hawajawahi elewana.

Mechi ya Jumapili itakuwa ya 86 kukutanisha miamba hawa, na ya kwanza kwa msimu huu. Gor Mahia kwa sasa iko katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 15, baada ya kushuka dimbani mara tano, pointi moja nyuma ya vinara Tusker FC wenye 16 baada ya mechi nane.

AFC Leopards inayonolewa na Mnyarwanda Casa Mbungo inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na pointi 15, baada ya kushuka dimbani mara nane. Ingwe imechukua ligi hii mara ya 13, ambapo mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1998.

Kwa upande wao, Gor Mahia wamebeba ndoo mara 18, ikiwa ni mara tatu mtawalia. Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza wa Mashemeji Derby kwa kocha Mwingereza Steve Polack na msaidizi wake Patrick Odhiambo. Casa Mbungo ni mzoefu wa derby.

Kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2016, Kogalo imekuwa ikiinyanyasa Ingwe. Msimu uliopita Gor Mahia ilishinda mechi zote walizokutana, ambapo mchezo wa kwanza ulimalizika kwa ushindi wa 2-0 na wa pili Ingwe akachukua kipigo cha 3-1.

Kwa bahati mbaya, ule msisimko wa derby hii siku hizi haupo kama ilivyokuwa zamani. Siku hizi mechi hizi zimekuwa ni sherehe ya wana wa Ogallo. Mara nne mtawalia kicheko kimekuwa hakikauki kwenye nyuso za mashabiki wa Gor Mahia.

Hata wanapoelekea kwenye mchezo huu ambao utakuwa wa kwanza kwa Dan Shikanda kama mwenyekiti wa Ingwe, Chui anajua kuwa shughuli haitakuwa rahisi. Chui ameingia baridi na ana sababu ya kufanya hivyo, kwa sababu ya hukumu ya historia.

Katika michezo mitano iliyopigwa kwenye kipindi cha miaka tisa ya hivi karibuni imeshuhudia matokeo ya sare. Sare ya 0-0 ilishuhudiwa miaka sita iliyopita (2013). Kukafuatia matokeo ya 2-2 kati ya Agosti 2013 na Julai 2014.

Mabao ya Ingwe katika sare ya kwanza ya 2-2 iliyopigwa mwaka 2013 wafungaji walikuwa ni Paul Were na Noah Wafula. Mabao ya Kogalo yaliwekwa kambani na David Owino na Dan Sserunkuma. Mwaka 2014, Sserunkuma alitupia mawili kambani katika dakika ya 43 na 47.

 

CHUNGU YA DERBY

KAMA ilivyo kwa derby nyingi, kuanzia ile ya Dar es Salaam, El Classico, Manchester, North London Derby, Super Classico ya Boca Juniors na River Plate, Mashemeji Derby au Nairobi au Dala Derby nayo huwa na chungu yake, vurugu

Machi 23, mwaka 2012, kundi la mashabiki wa Gor Mahia walianzisha vurugu baada kiungo Ali Abondo kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia rafu mbaya aliyomchezea mchezaji wa Leopards, Amon Muchiri.

Gor Mahia walifungiwa kutotumia viwanja vya Nyayo na Moi Kasarani katika msimu wote wa 2012 na bodi ya uongozi wa viwanja nchini. Kabla ya hapo, katika sherehe ya Mashujaa ya mwaka 2011 mashabiki wa Ingwe walisababisha kuvunjwa kwa mchezo wa robo fainali ya FKL Cup. Kuvunjwa kwa mchezo huo kulikuja baada ya mashabiki hao kuanza kuwarushia chupa waamuzi wa pembeni na vitu mbalimbali, wakionyesha kuchukizwa na bao safi lililofungwa na Moses Odhiambo aliyeunganisha kwa kichwa, ikabu iliyochongwa na Moses Otieno. Gor Mahia walitwaa taji hilo.

 KITENDAWILI CHA E-TICKETING

Kuelekea mchezo wa Jumapili, Gor Mahia ambao ni wenyeji katika mchezo huo, wamejipanga kutatua kitendawili cha mfumo wa kielektroniki wa kununua tiketi kwa kurahisisha utaratibu huo kwa mashabiki.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa Gor, Omondi Aduda ni kwamba, wamejipanga kuhakikisha kila mtu mwenye simu ya mkononi anapata urahisi wa kununua tiketi ambapo tayari klabu imetoa maelekezo kuhusu matumizi ya USSD kuepuka matatizo ya nyuma.

 “Tumekuwa na ugumu huko nyuma. Mashabiki wetu walipata tabu kununua tiketi hizi, katika michezo.