Mashabiki waanza kumiminika Taifa

Muktasari:

Kuanza kuchezwa saa 12:00 jioni Mchezo huo, inaweza ikawa moja ya sababu iliyopelekea mashabiki kushindwa kufika mapema uwanjani.

MASHABIKI wa soka hususani wale wa Yanga wameanza kumiminika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam japo ni tofauti na ilivyokuwa Jumapili iliyopita kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi, timu yao ilipocheza na Kariobang Sharks uliomalizika kwa sare ya 1-1.
Yanga inachea leo Jumamosi jioni dhidi ya Township Rollers  kwenye Uwanja wa Taifa katika Mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tofauti na Mchezo uliopita hadi muda huu tayari mashabiki walikuwa wameujaza Uwanja kwa sehemu kubwa huku nje kukiwa na kundi kubwa.
Kuanza kuchezwa saa 12:00 jioni Mchezo huo, inaweza ikawa moja ya sababu iliyopelekea mashabiki kushindwa kufika mapema uwanjani.
Nje ya Uwanja wa Taifa, wachuuzi wa jezi walikuwa wakiuza jezi mpya za klabu hiyo, japo wanunuzi hawakuwa wa kutosha kama ilivyokuwa Jumapili iliyopita.