Mashabiki wa Samatta waiteka mitandao ya Aston Villa

Muktasari:

Samatta katika akaunti yake ya Instagram ya Samagoal77 ina wafuasi 1.2milioni karibu sawa na idadi ya watu wa mji wote wa Birmingham.

London, England. Usajili wa Mbwana Samatta umekuwa ni neema katika mitandao ya kijamii ya klabu ya Aston Villa kwa kupata wafuasi wengi.

Mtandano wa https://www.birminghammail.co.uk umeripoti kuwa kuna jambo kubwa duniani la kuhofia kuhusu Aston Villa, Samatta atauweka mji wote mfukoni baada ya kukamilisha uhamisho huo jana wenye thamani ya pauni 10 milioni.

Samatta katika akaunti yake ya Instagram ya Samagoal77 ina wafuasi 1.2milioni karibu sawa na idadi ya watu wa mji wote wa Birmingham. Hiyo si jambo la kushangaza kwa sababu mshambuliaji huyo ni moja wa Watanzania vijana wenye ushawishi mkubwa katika miaka ya karibuni.

Mafuriko hayo wa wafuasi katika akaunti ya mitandao ya Aston Villa yamethibika wakati wa utambulisho wa Samatta alipata like 79,798 na Comment 16598.

Wakati utambulisha wa kipa mkongwe Pepe Reina wa Hispania alipata Like 34,893, Comment 611, wakati Danny Drinkwater alipata like 40678, comment 641.

Ukurasa huo wa Aston Villa kabla ya taarifa za Samatta kutua ulikuwa na wafuasi 540000 wanaofuatilia lakini baada ya habari za Samatta sasa umefikia wafuasi 600,000.

Samatta mwenye miaka 27, alianza kucheza soka Simba SC baadaye akajiunga na TP Mazembe kabla ya kuibukia  Genk mwaka 2016.

Samatta amefunga mabao 76, katika mechi 191 alizocheza Genk, pia ni nahodha wa Tanzania akiwa amefunga mabao 18 katika mechi 51 alizocheza.

Pia, alifunga bao dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa mwanzoni mwa msimu huu.

Samatta anaweza kuwapa Villa kile walichokikosa baada ya kuumia kwa mshambuliaji wake Wesley ambaye atakaa nje kwa msimu wote uliobaki.

Samatta anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa Villa Park mwezi huu baada ya Danny Drinkwater aliyechukuliwa kwa mkopo kutoka Chelsea na mkongwe Pepe Reina kutoka AC Milan.