Martial atoa ya moyoni Trafford

Muktasari:

Martial alisema falsafa ya kocha huyo kumpanga katika safu ya mshambuliaji asilia, imerejesha makali yake Man United.

London, England. Anthony Martial amesifu mbinu za kocha wa muda wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer.

Mchezaji huyo alisema ana furaha kucheza chini ya nguli huyo wa zamani wa timu hiyo kulinganisha na bosi wake wa zamani Jose Mourinho.

Martial alisema falsafa ya kocha huyo kumpanga katika safu ya mshambuliaji asilia, imerejesha makali yake Man United.

“Ni rahisi kucheza katika mfumo anaotufundisha kuliko ule wa Jose Mourinho,”alisema mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Martial hakuwa chaguo la Mourinho Man United na mara kwa mara walikuwa na msuguano uliotoa nafasi kwa klabu ya Juventus kutuma maombi ya kumsajili, lakini kocha huyo aliweka ngumu kabla ya kufukuzwa kwa matokeo mabaya.