Mapunda aona ugumu wa kiatu cha dhahabu VPL

Saturday September 19 2020

 

STRAIKA wa Dodoma Mji, Peter Mapunda amesema kwa namna msimu huu  ulivyoanza na ushindani, unampa picha ya kuwa makini kuhakikisha anajitengenezea heshima kabla ya ligi kuchanganya.

Mapunda amesema anauona ni msimu ambao utaibua uwezo wa wachezaji wengi kupambania timu zao, kuhakikisha zinakuwa kwenye mazingira yakutoshuka daraja hasa timu nje ya Simba,Yanga na Azam FC.

"Hii inatokana na msimu ulioisha kuziweka timu nyingi kwenye presha ya kushuka ndio maana mwanzo umekuwa mgumu, kwani kila mtu anapigania usalama wake wa kujiweka sawa mapema"

"Pia kuna ushindani kwa sisi washambuliaji kupigania kiatu cha dhahabu, baada ya kuchukua mara tatu mfululizo wageni kutoka timu ya Simba, alianza Okwi akafuata Kagere mara mbili mfululizo,"amesema Mapunda.

Amesema baada ya msimu ulioisha kumaliza na mabao 12 anahitaji kuvunja rekodi hiyo nakuweka  nyingine ambayo itamuingiza kwenye ushindani wa kuwania kiatu cha dhahabu.

"Kwanza msimu huu ushindani wa kuchuakua kiatu cha dhahabu utakuwa mkubwa zaidi kwasababu timu zimesajili, huku Simba na Yanga zikileta mastaa wengi zaidi wa kigeni ambao na wao watataka kuonyesha kitu, hilo ni jambo zuri kwetu kwani litaongeza ushindani,"amesema Mapunda.

Advertisement

Advertisement