Mangala ajifunga miaka miwili Valencia

Wednesday August 14 2019

 

By Matilda Tarimo

Klabu ya Valencia imefanikiwa kusamsajili kwa mkataba wa miaka miwili beki wa kati Eliaquim Mangala kutoka Manchester City.

Mfaransa huyo mwenye miaka 28, mara ya mwisho kuichezea City ilikuwa Januari 2018, lakini alifanikiwa kuongeza mkataba wa mwaka moja utakaomalizika Machi 2020.

Alipatwa na majeruhi katika muda wake mfupi aliocheza kwa mkopo Everton mwezi Februari 2018, pia alishawahi kucheza kwa mkopo wa muda mrefu Valencia katika msimu wa 2016-17.

Mangala ambaye ameichezea timu ya taifa ya Ufaransa michezo nane mwaka 2016, alijiunga na City akitokea Porto kwa dau la pauni 32milioni mwaka 2014.

Advertisement