Manara awapiga kijembe Yanga waige mfumo Simba

Muktasari:

Manara kikubwa ninachopenda kuwashauri watani zangu ni kuwaomba wapunguze marumbano wawe kitu kimoja na waingie katika makubaliano ya kuingia katika muundo wa muwekezaji ili kuondokana na changamoto ya kumtegemea mtu mmoja

 AFISA Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amewataka viongozi wa Yanga pamoja na wanachama wa klabu hiyo kuachana na dhana ya kumuamini mtu mmoja kuwa  pekee ndiye anaweza kuiendeza klabu hiyo badala yake amewataka kuamini mfumo.
Akizungumza Dar es Salaam leo Jumatano  alisema naamini kama Yanga haiwezi ikaenda bila Mwenyekiti wao Yusuph Manji na kuweka wazi kuwa wanachama na viongozi wanatakiwa kuangalia maslahi ya timu na sio wao binafsi.
Alisema kama wataingia katika mfumo wa hisa na kuuamini muundo huo basi hata muwekezaji atakaeingia hapo hata akitoka, mfumo alioukuta atauacha na mambo mengine yataendelea kama ilivyopangwa.
"Sisi tunamuwekezaji wetu kila mmoja anamfahamu ameingia hapo baada ya wanachama na viongozi kukubaliana kuingia katika mfumo huo. Hivyo muundo walionao sasa hata muwekezaji akitoka basi atakayeingia atafuata kilichoachwa," alisema.