VIDEO: Manara awapa mzuka mashabiki Simba

Muktasari:

Manara amesema wako makini kuelekea mchezo huo na mpaka sasa hakuna taarifa mbaya ya kuugua kwa mchezaji yoyote.

Simba imebakiza masaa machache kuingia uwanjani na msemaji wa timu hiyo, Haji Manara ametua na kusema wako sawa.

Manara ambaye amefika jana amesema muda huu wachezaji wao wanapata chakula cha mchana na baadaye kupumzika kidogo kisha kuelekea uwanjani.

Manara amesema wako makini kuelekea mchezo huo na mpaka sasa hakuna taarifa mbaya ya kuugua kwa mchezaji yoyote.

Amesema malengo ya Simba ni makubwa kuhakikisha wanatinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.