Manara: Simba hii inastahili ubingwa

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kikosi chao kilistahili kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara na hata Kombe la Shirikisho (FA), ambalo wapo hatua ya nusu fainali na kesho Jumapili watacheza dhidi ya watani zao Yanga.

Manara amesema kikosi cha watani wao, ambacho kilitwaa ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo na kufanya vizuri katika mashindano mengine walikuwa na wachezaji wa maana wenye viwango vya juu kama Donald Ngoma, SaimonMsuva, Thabani Kamusoko.

Amesema wapinzani wao kwa sasa wana wachezaji wa kawaida tofauti na wachezaji wa Simba kwa maana hiyo wanatakiwa kutulia na kufanya maamuzi sahihi ili kuwa na kikosi bora ambacho kitaleta ushindani.

"Angalia kikosi cha Simba kwa sasa kina mchezaji kama Luis Jose, Cletous Chama, Francis Kahata, Meddie Kagere na wengineo hivi hawa kweli wakiwa fiti na kucheza katika viwango vyao vya juu tunaweza kufungwa na Yanga au kushindwa kutwaa makombe mengi zaidi tuliokuwa nayo msimu huu,"

"Katika kuhakikisha tuna kikosi bora msimu huu tumepania kulipiza kisasi mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, dhidi ya Yanga kwani mechi mbili za ligi tumeshindwa kupata pointi tatu dhidi yao," amesema Manara.