Man Utd, Man City zagombea mchezaji

Sunday September 9 2018

 

Manchester United na Manchester City zimeingia katika mvutano wa kuwania saini ya nyota wa Wolves, Ruben Neves.

Imefahamika kwamba Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola yupo tayari kutoa kiasi cha Pauni 60 milioni ambazo zinahitajiwa na klabu ya Wolves ili wamuuze Ruben.

Pia, kocha wa Manchester United Jose Mourinho amepewa rungu na viongozi wake ambao wamesema kwamba wapo tayari kutoa kiasi hicho cha pesa ili kumsajili mchezaji huyo.

Mourinho amekuwa akimwangalia mchezaji huyo kwa muda sasa na anaona anafaa katika kikosi chake.

Na baada ya kuona kwamba Guardiola amemfungia kazi, ameamua kuingia vitani kwa kasi  akiamini kwamba atamsajili mara baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili la Januari.

Advertisement