Makambo ameshindikana

Muktasari:

  •       Pamoja na Eliud Ambokile wa Yanga kuwa kinara kwa kufunga mabao nane, ameitazama kasi ya Makambo na kudai kuwa amempa changamoto ya kujitathimini upya.

STRAIKA wa Mbeya City, Eliud Ambokile ndiye anayeongoza kwa mabao katika Ligi Kuu akiwa amecheka na nyavu mara tisa, akiwafunika nyota wa Simba na Yanga, lakini anakiri hakuna mchezaji anayempasuSTRAIKA wa Mbeya City, Eliud Ambokile ndiye anayeongoza kwa mabao katika Ligi Kuu akiwa amecheka na nyavu mara tisa, akiwafunika nyota wa Simba na Yanga, lakini anakiri hakuna mchezaji anayempasua kichwa kama Mkongomani, Heritier Makambo akidai jamaa ameshindikana kwa kasi yake ya kutupia.a kichwa kama Mkongomani, Heritier Makambo akidai jamaa ameshindikana kwa kasi yake ya kutupia.

Ambokile alisema Makambo anayekipiga Yanga na straika tishio wa Simba, Meddie Kagere ndio anaowahofia kupindua meza wakati wowote kwenye mbio za Kiatu cha Dhahabu kutokana na kasi yao.

Straika huyo aliyekuwa akitajwa kuwindwa na klabu kubwa katika dirisha hili la usajili, alisema amegundua kuwa Makambo na Yanga nzima wana umoja na kampeni ya timu nzima ni kutaka kuonyesha uwezo wao licha ya kukabiliwa na ukata kitu kinachomtisha.

“Ukiiangalia Yanga unagundua wana dhamira ya kufanya kitu cha tofauti kwa msimu huu, Makambo anaendana na kasi ya klabu yake, hilo nalichukulia kama changamoto ya kuongeza juhudi na ushirikiano wa wachezaji wenzangu tutafika mbali,” alisema.

Baada ya kumaliza kumuelezea Makambo alimgeukia Kagere wa Simba kuwa anajua kulazimisha mashambulizi kutokana na mwili wake kuwa fiti, pia anamuona ni straika, ambaye muda wote anafunga.

“Makambo na Kagere ni wazoefu kwangu, pia wanajua wanachokifanya, siwezi kuona kuongoza kwa kufunga mabao tisa nimemaliza kila kitu, ndio maana nimeusoma ubora wao, ili nijue namna ya kupambana nao.

“Lakini kuna Emmanuel Okwi, ambaye uwezo wake unajulikana, nitaendelea kupambana nipo tayari kwa lolote litakalotokea, kama nitachukua kiatu ama hao niliowataja pia nitawatakia heri,” alisema Ambokile.

Kuhusu tetesi za kutakiwa na Yanga alisema kama mabosi wa klabu hiyo wanamtaka basi wanatakiwa kufuata sheria.

“Ikitokea nikaenda Yanga ama Simba, nitakuwa nimejiamini katika nafasi yangu ya kucheza, siwezi kuwahofia wakati najua soka ni kazi yangu, lazima nitapambana ili niwe kama wao, ila muhimu wanaonihitaji wafuate sheria na taratibu tu,” alisema.