VIDEO: Maisha ya Yanga yamkuna Fei Toto kinoma

Saturday August 11 2018

 

By Khatimu Naheka

Morogoro. Kiungo mpya wa Yanga, Feisal Salum 'Fei toto' amesema tangu ajiunge na timu hiyo anafurahia maisha yake mpya ndani ya klabu hiyo.

Feisal amesema mpaka sasa maandalizi yao yako vizuri na kwamba wanataka kufanya vizuri katika Ligi Kuu msimu huu.

Kiungo huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea JKU ya Zanzibar amesema ushindani wa namba katika kikosi hicho ni mkubwa, lakini hana wasiwasi na uwezo wake akimuachia kocha anajua ataitumikiaje klabu yake.

Amesema kikosi chao kitapambana kiukweli kuhakikisha wanatimiza malengo ya yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kumaliza kwa heshima katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Advertisement