Magori abebeshwa zigo la kocha msaidizi

Muktasari:

Simba haija ajiri kocha msaidizi kwa zaidi ya miezi
mitano tangu ilipoachana na Mrundi Masoud Djuma ili amsaidie Mbelgiji Patrick Aussems.

Dar es Salaam. Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori amepewa jukumu zito la kumsaka kocha msaidizi wa timu hiyo atakayeziba pengo la Mrundi Masoud Djuma na kumsaidia Mbelgiji Patrick Aussems.
Tangu msimu wa Ligi Kuu Bara uanze, Simba imekuwa haina
kocha msaidizi baada ya kuachana na Mrundi, Masoud Djuma
aliyekuwa anahudumu nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji
amesema uongozi umeacha mchakato wa kumsaka mrithi wa Djuma mikononi mwa Magori wakiamini ataweza kuwaletea mtu sahihi.
"Jambo lingine ambalo tumelijadili kwenye kikao cha bodi ya
klabu ni suala la kocha msaidizi ambalo tumekubaliana tuliache kwa Mtendaji Mkuu (CEO) Magori,"alisema Mo Dewji.
Ikumbukwe kuwa huyu Patrick Aussems tulimpata kupitia usaili
ambao ulifanywa na jopo la makocha na wataalamu hivyo hata kwa kocha msaidizi, CEO atashirikiana na wataalam ambao
tutawaandaa," alisema Dewji