Madrid wajanja, Mbappe ategwa

Saturday February 15 2020

Madrid wajanja, Mbappe ategwa,PARIS Saint-Germain, Kylian Mbappe,Real Madrid,

 

PARIS, UFARANSA. PARIS Saint-Germain inapambana kwa nguvu zote kumbakiza Kylian Mbappe baada ya kuona Real Madrid wamekoleza moto wa kumsajili na kwamba wanahofia kumtuliza kwa Pauni 100 milioni.
PSG wao wamepanga kumpa Mbappe mshahara mkubwa kama ambavyo wamekuwa wakilipwa mastaa wa nguvu kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ili kubaki kwenye chama lao kwa muda mrefu.
Taarifa za kutoka Hispania zinadai kwamba PSG wapo tayari kumfanya Mbappe kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani ili kuwakomesha Madrid wanaosumbuka kutaka saini yake.
Lakini, shida inakuja sehemu moja tu, Madrid wamemweka staa huyo kwenye mpango wao na mipango ni kumshawishi asisaini dili jipya huko Paris, ili wao wamchukua mwakani kwa dau litakalopungua hadi Pauni 100 milioni.
Mbappe kwa sasa analipwa mshahara wa Pauni 125,000 mkataba wake utafika tamati 2022, lakini ikifika mwakani thamani yake itashuka kwa sababu atakuwa amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba huo na hapo Madrid watakuwa na uwezo wa kumsajili kwa dili lisilozidi Pauni 100 milioni.
Utakapobaki mwaka, PSG hawatakuwa na namna nyingine zaidi ya kumpiga bei tu kama atagoma kusaini dili jipya ili kukwepa kumpoteza bure. Mabingwa hao wa Ufaransa wanataka kumtuliza kwa mshahara mrefu ili ilimlipe kama wanavyolipwa Ronaldo na Messi, Pauni 510,000 na Pauni 541,796 kwa wiki mtawalia.
Tangu Neymar atue PSG, Nike wamenogewa na kupandisha mkataba wake wa udhamini wa jezi kwenye timu hiyo, kutoka Pauni 21 milioni kwa mwak hadi Pauni 63 milioni huku mauzo ya jezi yakiongezeka zaidi.

Advertisement