Machester City wamng’oa Kocha Brighton

Muktasari:

Mwenyekiti wa Klabu ya Brighton and Albion, Tony Bloom amesema  kwenye taarifa yake iliyotumwa kwenye mtandao wa timu hiyo, kuwa  Kocha Hughton amefanya kazi nzuri kwa miaka minne iliyopita na kipindi cha nusu mwaka huu

London, England. Uongozi wa timu ya Brighton and Albion umemtimua kocha wa timu hiyo, Chris Hughton siku moja baada ya kufungwa mabao 4-1 na Manchester City ambayo imetwaa Ubingwa wa England msimu huu wa 2018/2019.

Kocha huyo ametimuliwa mapema leo Jumatatu licha ya timu hiyo kunusurika kuteremka daraja msimu huu.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Tony Bloom amesema  kwenye taarifa yake iliyotumwa kwenye mtandao wa timu hiyo, kuwa  Kocha Hughton amefanya kazi nzuri kwa miaka minne iliyopita na kipindi cha nusu mwaka huu hata hivyo wamelazimika kumuondoa kutokana timu hiyo kutofanya vizuri.

“Huu umekuwa moja ya uamuzi mgumu kwa klabu yetu niliotakiwa kuufanya nikiwa mwenyekiti wa Brighton, lakini imetulazimu kwa jinsi ambavyo timu imekuwa ikifanya vibaya katika nusu ya msimu huu ulioisha.” Alisema mwenyekiti huyo wa klabu.

Aliongeza kuwa ushindi wa kusuasua wa timu hiyo imekuwa moja ya sababu zilizoufanya uongozi wa timu hiyo kumtimua kocha huyo klabu hapo.

Hata hivyo uongozi wa timu hiyo umesema kwamba mchango wake utakumbukwa na mashabiki pamoja na wafanyakazi wa klabu hiyo, huku wakimtakia maisha mema kwenye utendaji wa majukumu yake klabu atakayokwenda kuifundisha.