Mabaharia; Aliyemshauri Wema kujikondesha ni adui wa umma

Tuesday September 10 2019

 

By Luqman Maloto na Dk Levy

NANI aliyethubutu kumshauri Wema Sepetu “Tanzania’s Sweetheart” awe kimbaumbau na kuupukutisha ule ‘mshepu’ wake pendwa?

Mabaharia wametoa hukumu! Halafu Harmonize ndio nini kuoa bila kumwalika Diamond, alimwona anakula sana? Yule Juma K Juma yule! Njoo kijiweni, Dk Levy na Luqman Maloto wanayajenga!

LEVY: Vipi lakini uko poa ndugu yangu wa damu kabisa?

LUQMAN: Bur’daaani kabisa Daktari. Unajua nini? Kuna kamstari kembamba mno kati ya upendo na chuki.

LEVY: Aaaah hilo unalijua leo? Wangeweka mstari mpana mwanadamu asingepata akili ya kutengeneza pesa. Mpaka sasa tungeishi kwa ujima ule wa ‘bata tredi’ nakupa magimbi unanipa chaja ya kobe.

LUQMAN: Harmonize ni wa kumnyima mwaliko wa harusi Diamond kweli? Kwani Diamond anakula sahani ngapi za ubwabwa?

Advertisement

LEVY: Umejuaje? Mimi sifuatilii mambo hayo kwa sasa. Niko bize na mabaharia wa Taifa Stars hasa baharia mkuu Kaseja Juma. Hao madogo nimewapa breki kimtindo maana ishu zao kama za Alinacha.

LUQMAN: Halafu Harmonize na mkewe ndio nini kuifanya mechi ya Taifa Stars na Burundi ndio fungate yao Taifa?

LEVY: Leo umeamua kunivuruga. Maana sina ninalojua kuhusu hizo makitu. Kwa hiyo fugate wamefanyia kwa Mchina?

LUQMAN: Halafu Daktari, nimegundua Wema ‘kiki’ yake imeondoka na ule mshepu wake. Tangu ajigeuze kimbaumbau habambi kabisa. Wabongo wanaweza kukushobokea, ukafikiri wanakushobokea wewe na pirika zako, kumbe mshepu! Si unamkumbuka Mariam Biriani?

LEVY: Aiseeee pia ule mshepu ulikuwa umehifadhi nyota yake ya kupendwa nadhani. Toka awe kimbaumbau hata likes na comments kwenye page yake insta ni chache kama nywele za Mzee Cheyo.

LUQMAN: Yaani Wema bila ule mshepu hata Ebitoke anamburuza. Yaani Amber Rutty anakimbiza kuliko Wema. Aliyemshauri Wema kuupukutisha ule mshepu wake ana roho mbaya kama tindikali, katili kuliko Kibweteere!

LEVY: Niko kwenye maandalizi ya kufungulia kesi ya mshauri wa Wema. Yaani kaondoa moja ya maliasili ya taifa. Wema sio Wema bila ule msambwanda. Kweli upendo na chuki hutenganishwa na kamba nyembamba sana. Mungu yupo atatulipia. Kweli Wema wa kufanana msambwanda na Johari au Chuchu Hans kweli?

LUQMAN: Aliyemshauri Wema ajikondeshe amejitafutia moto wa kiyama bila sababu. Hivi anajua ameumiza watu wangapi? Leo hii nchi ikipungukiwa watalii tutalaumu Bodi ya Utalii wakati kuna binadamu amekiteketeza kivutio cha utalii kwa ushauri wake wa hovyo. Natamani Wema angekuwa hifadhi ya taifa ili aliyemshauri Wema akondeane ashtakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi ya umma.

LEVY: Wema na ule Msambwanda wake angeenda Sauzi, ndege yetu ingeachiwa kiulaini. Mshepu wa Wema na mapango ya Amboni mimi naona bora shepu ya Wema. Ni zaidi ya nyayo za yule pimbi wa kale aliyekatiza mitaa ya Kondoa Irangi miaka milioni 3 iliyopita. Aliyemshauri Wema aondoe kivutio chetu cha utalii maungoni mwake alaaniwe yeye na kizazi chake. Kila akizaa watoto wawe wembamba kama toothpick.

LUQMAN: Kwani Dk Levy wewe ni baharia mwenzetu?

LEVY: Mimi ni baharia msomi mwenye hela. Ujue kutofautisha. Hawa mabaharia wa Kibongo wengi wanajiita mabaharia baada ya kupigika kinoma ili kwa madem wapite kwa ganda la ndizi triiiiii mpaka Macca. Mimi baharia wa moyo ile kiroho safi yaani. Siyo baharia njaa njaa kapuku mwenye ukame wa pesa kwa mfuko.

LUQMAN: Hizo stori zako hazina mafasi hapa. Kwa kifupi kikao chetu cha mabaharia kimeshaamua kuwa aliyemshauri Wema kuondoa mshepu wake ni adui wa umma. Tulikuwa tunajiuliza mbona Bongo Movie siku hizi watalii wamekatika? Kumbe kivutio kikuu kimetoweka.

LEVY: Kabisa soko la filamu limeanguka baada ya Wema kuleftisha shepu lake. Wasanii wa filamu wanapaswa kumsaka mchawi wao ambaye ni yule dudumizi aliyetoa huo ushauri wa kijinga. Unajua kuna vitu ukikosea unaharibu mpaka tabia nchi. Wema... Wema... Wema... Nimekuita mara tatu. Kwa nini lakini umeamua kutuondolea hitaji letu la moyo na rasilimali ya taifa letu?

LUQMAN: Mwisho nakupa nafasi ya kumpongeza Juma K Juma kwa kazi nzuri. Pongeza wachezaji wote.

LEVY: Juma Kaseja yule ndo maana halisi ya Tanzania One. Ujue sio kila kipa apewe jina la Tanzania One. Hawa wengine waitwe golikipa tu inatosha. Utulivu wa Kaseja kwenye penati unafanya mpigaji awe na worry yenye stream ndani yake inayofanya miguu ifent not to that extent kwenye spinal code kabla ya kuslide kama tiles na kujikuta anampelekea Juma mikononi. Kwako Chacha Maginga!

Advertisement