Lwandamina agoma kuangalia mechi za Yanga

Thursday September 12 2019

 

By Khatimu Naheka

Kikosi kamili cha Zesco ya Zambia kimewasili nchini tayari kwa kuvaana na wenyeji wao Yanga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Akizungumza na mara baada ya kuwasili kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina amesema wako tayari kukutana na Yanga lakini akathibitisha kwamba hakupoteza muda kutafuta mikanda ya wapinzani wao.
Lwandamina ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga amesema Zesco imejiandaa kukutana na Yanga wakitanguliza ubora wao.
Lwandamina amesema anafahamu kwamba Yanga ina kikosi kipya,uongozi mpya na benchi la ufundi jipya huku mmoja pekee anayemfahamu ni aliyekuwa msaidizi wake kocha Noel Mwandila.
Kocha huyo mpole amesema hakutumia muda mrefu kutafuta mikanda ya Yanga kutokana na ingeweza kumchanganya ingawa msaidizi wake mmoja aliangalia mechi moja pekee ya Ligi Kuu Bara ambayo Yanga ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.
Aidha kocha huyo amesema kikosi alichokuja nacho anaaminj kitaweza kumpa matokeo waliyojipangia kiyatafuta mbele ya Yanga.

Advertisement