Lipuli na wengine watatu washuka, Mtibwa chupuchupu

Muktasari:

Matokeo ya michezo mingine; Tanzania Prisons 2-2 Azam, Coastal Union 0-1 JKT Tanzania, Polisi Tanzania 1-2 Simba, Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar, Singida United 0-2 Biashara United.

HATIMAYE Ligi Kuu imemaliza leo Jumapili, Julai 26, 2020 huku timu nne zikiaga rasmi ligi hiyo baada ya michezo 10 kupigwa viwanja tofauti.

Singida United ilikuwa timu ya kwanza kuaga ligi hiyo, na baada ya michezo ya leo, Ndanda FC imefuata kutokana na kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Mbao FC.

Mbao FC licha ya kupata ushindi huo imemaliza nafasi ya 15 na sasa itacheza na Ihefu FC hatua ya mtoano huku Mbeya City iliyoichapa 3-0 KMC itacheza na Geita Gold FC.

Lipuli FC nayo imeshuka daraja baada ya kushika nafasi ya 18 ikiwa na alama 44 kutokana na kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Yanga.

Alliance FC licha ya ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Namungo FC Uwanja wa CCM Kirumba, haikusaidia kitu baada ya kumaliza nafasi ya 17 ikiwa na alama 45.

Ushindi wa mabao 2-1 iliyoipata Mtibwa Sugar nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting, imewaokoa kutoka nafasi ya 15 na kupanda nafasi moja iliyowabakisha salama ligi hiyo.

Matokeo ya michezo mingine, Tanzania Prisons 2-2 Azam, Coastal Union 0-1 JKT Tanzania, Polisi Tanzania 1-2 Simba, Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar, Singida United 0-2 Biashara United.