Lampard amuita Klopp ‘mnafiki’ kwa kuwakosoa

Tuesday September 15 2020

 

London, England. Kocha Frank Lampard amemtaja Jurgen Klopp kama ‘mnafiki’ baada ya kuikosoa Chelsea katika matumizi yake ya usajili wa msimu huu.

Lampard alisisitiza kuwa matumizi yao ya Pauni 200 milioni imewafanya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kushituka kwani walikuwa katika kifungo wakati wanatwaa ubingwa.

Kocha wa Reds, Klopp ilishindwa kushindana na Chelsea katika kutoa kitita cha Pauni 48 milioni kumsajili Timo Werner na kudai kuwa timu yake haiwezi kuendeshwa kama timu nyingine za ligi hiyo.

Lakini Lampard alisema: “Hakuna sababu ya msingi kuanza kufanya hesabu. Tunajua kwamba Liverpool ilitumia fedha kwa kiasi kikubwa misimu iliyopita.

“Kwa Liverpool, ni hadithi nzuri ya klabu katika mika aminne na nusu tangu Jurgen Klopp awepo, na walikubali kufanya matumizi makubwa kwa ajili ya kutafuta mafanikio.

“Ukweli ni kwamba klabu nyingi ambazo zinafanikiwa kutwaa ubingwa ujue wazi kuwa ni lazima zilifanya makubwa sokoni kwa kutoa fedha nyingi pia.

Advertisement

“Unaweza kwenda kuangalia wachezaji wa Liverpool, Virgil Van Dijk, Alisson, Fabinho, Naby Keita, Sadio Mane, Mo Salah, wachezaji muhimu ambao walikuja kwa gharama. “Liverpool imefanya yote hayo katika vipindi tofauti.”

Advertisement