Kwenye mdundiko Ethiopia wako vizuri!

Saturday November 16 2019

TIMU - soka - Wanawake -Ethiopia-wachezaji-mwanasport-MwanaspotiSoka-MwanaspotiGazeti-

 

By Doris Maliyaga

TIMU ya soka ya Wanawake ya Ethiopia iliweka wazi kwa vitendo kuwa wao ni hatari kwenye mpango mzima wa kuimba na kucheza ngoma za asili.

"Hizi kule ni sawa na ngoma za asili za tamaduni tofauti lengo ni kupeana moyo tu ili tufanye vizuri,  "alisema kiongozi mmoja wa Ethiopia.

Wachezaji hao waliwashawishi kujumuika na viongozi wa soka lao pamoja na benchi la ufundi wakaimba na kucheza pamoja.

Waliimba nyimbo tofauti za kitamaduni za kwao yaani kama ilivyo mdundiko kwa watu wa kabila la wazaramo na waluguru au zile za kimasai.

Wakati wanaimba,  walizunguka duara, kisha mchezaji mmoja mmoja alianzisha nyimbo yake na wengine wanaitikia na mmoja wao hadi wawili waliingia kati na kucheza.

Ilipendeza kwa kweli wengine walitingisha mabega na viuno na wengine walipiga makofi huku wakicheza.

Burudani hiyo ilidumu kwa kipindi cha takribani dakika 10, ambapo watu wao wa benchi la ufundi walisema kama kuweka morali.

Timu hiyo,  inajiandaa na mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Kenya mechi itachezwa saa 8: 00 mchana Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Advertisement