Kwa Molinga bado nne tu

Muktasari:

Kama Molinga atautumia vizuri mchezo wao wa keshokutwa Jumatatu dhidi ya KMC utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, huenda akapunguza pengo la mabao baina yake na Kagere na hata kuwafikisha nyota wengine waliopo juu yake kwenye orodha ya wafungaji mpaka sasa.

BAO lake dhidi ya Alliance jana limememfanya straika wa Yanga, David Molinga kufikisha la nne na kubakisha mabao manne tu kumnasa nyota wa Simba na kinara wa orodha ya wafungaji Meddie Kagere alioyepachika nane mpaka sasa.
Molinga aliyesajiliwa msimu huu kutoka DR Congo, ndiye kinara wa mabao wa Yanga kwa sasa akimzidi bao moja Patrick Sibomana ambaye jana alifunga bao la kwanza la timu yake na kumfanya afikishe matatu sawa na nyota wa klabu nyingine walio na mabao kama hayo.
Straika huyo mwenye 'mwili jumba', alianza kufunga mabao mawili dhidi ya Polisi Tanzania katika mechi iliyoisha kwa sare ya 3-3 kisha kufunga jingine moja mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania na jana tena kuongeza moja.
Hata hivyo katika mchezo wa jana dhidi ya Alliance kama mshambuliaji huyo angekuwa makini alikuwa anaondoka hata na hat trick kwani alipata nafasi nyingi lakini alipoteza, jambo lililowatibua mashabiki wachache waliokuwa na kiu ya kuona Yanga ikitoka uwanjani na ushindi mnono.
Kama Molinga atautumia vizuri mchezo wao wa keshokutwa Jumatatu dhidi ya KMC utakaopigwa Uwanja wa Uhuru, huenda akapunguza pengo la mabao baina yake na Kagere na hata kuwafikisha nyota wengine waliopo juu yake kwenye orodha ya wafungaji mpaka sasa.
Paul Nonga wa Lipuli ndiye anayemfuata Kagere kwa mabao akifunga saba, tatu zaidi na aliyonayo Molinga, huku akifuatiwa na Miraj Athumana wa Simba na Darueshi Saliboko wa Lipuli wenye mabao sita kila mmoja na kufuatiwa na Yufu Mhilu wa Kagera Sugar na Peter Mapunda wa Mbeya City waliofunga mabao matano kila mmoja mpaka sasa.
Kundi la webnye mabao manne linalomjumuisha Molinga lina wakali wengine kadhaa akiwamo Mathias Mdamu wa Mwadui, Samson Mbangula (Prisons), Awesu Awesu (Kagera Sugar), Waziri Junior (Mbao FC) na  Adam Adam (JKT Tanzania).

Ebu cheki hapo chini orodha ya wafungaji ilivyo kwa sasa;
WAFUNGAJI
8 Meddie Kagere (Simba)- Rwanda
7  Paul Nonga (Lipuli FC)
6 Daruesh Seif Saliboko (Lipuli)
   Athuman Miraj (Simba)
5 Yusuf Mhilu (Kagera Sugar)
   Peter Mapunda (Mbeya City)
4 David Molinga (Yanga)- DR Congo
   Gerald Mathias Mdamu (Mwadui)
   Samson Mbangula (Prisons)
   Awesu Awesu (Kagera Sugar)
   Waziri Junior (Mbao FC)
   Adam Adam (JKT Tanzania)
3 Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania)
   Lucas Kikoti (Namungo FC)
   Sadat Mohammed (Ruvu Shooting)
   Shaaban Idd Khamis (Coastal Union)
   Innocent Edwin (Biashara United)-Nigeria
   Obrey Chirwa (Azam)- Zambia
   Patrick Sibomana (Yanga)-Rwanda
2 Donald Ngoma (Azam FC)-Zimbabwe
   Jerry Tegete (Alliance FC)
   Paul Luyungu (Lipuli)
   Aziz Ismail (Tanzania Prisons)
   Abdulhalim Humud (Mtibwa Sugar)
   Hassan Kapalata (Mwadui FC)
   Edward Songo (JKT Tanzania)
   Emmanuel Charles Lukinda (Mbao FC)
   Dickson Daud (Mtibwa Sugar)
   Mohammed Mkopi (Polisi TZ)
   Jaffar Kibaya (Mtibwa Sugar)
   Frank Ikobela (Kagera Sugar)
   Martin Kiggi Luseke (Alliance FC)
   Idd Seleman Naldo (Azam)
   Serge Alain Nogues (KMC)- Ivory Coast
   Ayoub Lyanga (Coastal Union)
   Reliants Lusajo (Namungo FC)
   Nassor Kapama (Kagera Sugar)
   Danny Lyanga (JKT Tanzania)
   Bigirimana Blaise (Namungo)-Burundi
  Deogratius Anthony Kulwa (Coastal Union)
  Adili Buha (Tanzania Prisons)
  Shaaban Idd Chilunda (Azam)
  Haruna Chanongo (Mtibwa Sugar)