Kumbe mpinzani wa Mwakinyo ndo ticha wa Gigy Money

Thursday August 13 2020

 

By KELVIN KAGAMBO

Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi, mpinzani wa Mwakinyo kwenye mchezo pambano litakalopigwa kesho Agosti 14 ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, mkongo Tshibangu Kayembe alipokelewa na msanii wa Bongofleva, Gigy Money alipotua nchini.

Mapokezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jumanne usiku yalirekodiwa kwenye video zilizosambazwa mitandao ikimuonyesha Gigy Money akiwa na Tshibangu pamoja na meneja wa bondia huyo mbele ya waandishi wa habari huku Gigy akimzunguzia Tshibangu tena kwa kiingereza.

Baada ya video hiyo kusambaa Instagram na kwenye mitandao mingine ya kijamii kila mtu akaongea lake kuhusu mapokezi hayo huku wengi wakiamini huenda ni mbinu inayotumiwa na timu ya Mwakinyo kumzuzua mpinzani wake.

Sasa leo Agosti 13, 2020 Mwanaspoti ilimsaka Gigy ili atolee ufafanuzi ishu hiyo ambapo ameeleza alikwenda kumpokea kama kumpokea kama shabiki.

“Mimi napenda ngumi na Tshibangu ni moja ya watu ninaowafuatailia sana. Kwahiyo niliposikia anakuja Tanzania nikasema nikampokee kama shabiki yake.” ameeleza.Aidha, Gigy amedai kutokana na kwamba yeye ni mtu wa matukio ya mara kwa mara, amejikuta akipenda ngumi kwa sababu anapotazama huiba vitu viwili vitatu ambavyo huvitumia kwenyehayo matukio yake.

“Nishakwambia napenda ngumi, we mwenyewe si unaona nilivyokaa kingumi ngumi, kwahiyo nikimtazama mtu kama Tshibangu kuna vitu napata, kukwepa kwepa, kupiga jab right, jab left napata huko.” ameeleza.

Advertisement

Ikumbukwe umemalizika mwezi tu tangu Gigy Money atwangane makonde na aliyekuwa mpenzi wake, Mnaigeria Hunchy Huncho katika red carpet ya show ya msanii Zuchu ilitofanyika Mlimani City Dar es Salaam.

Advertisement