Kumbe ishu yote ya Simbu iko hivi

Muktasari:

  • Hata hivyo, tangu amemaliza mafunzo hayo, Simbu amekuwa kwenye wakati mgumu katika rekodi yake ya riadha ambapo mara mbili mfululizo ameshindwa kumaliza mbio akiwa Colombia na hivi karibuni katika mbio za New York City Marathoni, Marekani.

TANGU ametoka kwenye mafunzo maalumu ya kijeshi, Alphonce Simbu amekuwa katika kipindi kigumu kwenye mbio huku taarifa za chinichini zikieleza kuwa mafunzo hayo yameshusha kiwango cha nyota huyo wa mbio ndefu nchini.

Simbu ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alikuwa miongoni mwa nyota wa riadha waliokwenda kwenye mafunzo maalumu ya jeshi na walipomaliza walipata ajira.

Hata hivyo, tangu amemaliza mafunzo hayo, Simbu amekuwa kwenye wakati mgumu katika rekodi yake ya riadha ambapo mara mbili mfululizo ameshindwa kumaliza mbio akiwa Colombia na hivi karibuni katika mbio za New York City Marathoni, Marekani.

“Kilichonitokea ni kuanza kufanya mazoezi kwa nguvu sana, wakati nikiwa nimetoka kwenye mafunzo, hivyo nikajikuta nimeji ‘over training’,” alisema Simbu jana akiwa njiani kwenda Dar es Salaam kwa masuala binafsi.

Alisema aliharakisha kufanya mazoezi bila kufuata misingi mizuri, hivyo kujikuta akijiumiza na kupata majeraha ya ndani kwa ndani yaliyosababisha kupata maumivu ya misuli ya mguu wa kushoto.