Kotei awataka TP Mazembe

Friday March 22 2019

 

By Thobias Sebastian

Kiungo mkabaji wa Simba Mghana James Kotei amesema ili uwe bingwa lazima uwafunge mabingwa.
Kotei alisema hayo baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwapanga na TP Mazembe katika hatua ya robo fainali.
Alisema katika hatua kubwa kama ambayo tumefikia ya robo fainali ni lazima tukutane na timu yoyote yenye mafanikio katika mashindano haya.
"Tunatambua ukubwa na ugumu wa TP Mazembe na haswa kwenye hatua kama hii ya robo fainali, tunafahamu hautakuwa mchezo rahisi kwa upande wetu," alisema.
"Tumeshafahamu mpinzani wetu kikubwa benchi la ufundi litatupatia maandalizi sahihi kabisa ya kuelekea mechi hii ambayo tunaanzia nyumbani ili kupata matokeo mazuri mbele ya mashabiki zetu.
"Tunaomba mashabiki wote wa Simba wajitokeze kwa wingi kama ilivyokuwa katika mechi nyingine zote tilizocheza katika mashindano haya," alisema Kotei.

Advertisement