Kocha wa viungo, Riedoh aisikilizia Yanga

Thursday October 15 2020
kocha yanga pic

Dar es Salaam. Ni suala la muda tu kwa uongozi wa Yanga kumtambulisha kocha mpya, Cedric Kaze, ambaye anatua nchini leo.

Wakati hilo la kumsubiria Kaze atangazwe likingojewa kwa hamu, kocha wa viungo wa Yanga, Riedoh Berdien hayupo kwenye kikosi hicho kwa muda usiopungua wiki mbili.

Berdien alibainisha kuwa wengi wanaamini yupo Afrika Kusini, lakini kwa sasa yupo katika majukumu ya kitaifa.

“Watu wengi wanafahamu nipo Afrika Kusini, nipo Gambia katika majukumu ya timu taifa (Bafana bafana), na wiki iliyopita tulicheza mechi ya kirafiki na Congo na kuwafunga bao 1-0.

“Baada ya kumaliza majukumu yangu nitawasikiliza kwanza viongozi wa Yanga ili kujua mwenendo wa mkataba wangu ambao unamalizika Januari kama utaendelea au kusitishwa.

“Siwezi kufanya uamuzi wowote kwa sasa, nafasi kubwa nawapa Yanga, ambao nipo na mkataba nao wa miezi mitatu kabla ya kumalizika na wao baada ya kutoa uamuzi ndiyo nitakueleza, hizi klabu muda wowote unaweza kusitishiwa mkataba.

Advertisement

“Bado sijazungumza na kocha mpya ajaye Yanga, bado sijamfahamu ingawa nasikia atakuja Kaze, kama nitapata nafasi ya kuzungumza naye itakuwa vizuri kufahamu muelekeo,” alisema Berdien.

Katika hatua nyingine Berdien alisema amepata ofa za kuhitajika na baadhi ya klabu, lakini si nyingi kama zilivyokuwa timu za taifa ambazo zinahitaji kumpa kazi ya moja kwa moja.

Advertisement